• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Secondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Mipango Takwimu na Uuatiliaji
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

WILAYA YA MISSENYI YAPOKEA SETI ZA VITI NA MEZA 100 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO TIB

Posted on: February 9th, 2021

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi leo imepokea msaada wa seti 100 za viti na meza kwa ajili ya shule za sekondari wilayani hapa. Akisoma taarifa ya Hali ya Elimu  Wilayani hapa wakati wa hafla ya mapokezi wa samani hizo; Afisa elimu Sekondari Wilaya ya Missenyi  Bi Saverina Misinde amenukuliwa akisema kuwa Halmashauri ilituma maombi kwa wafadhili mbalimbali kuomba msaada wa vifaa vya ujenzi na Viti na Meza na Tanzania Investment Bank (TIB)  ni moja ya wafadhili waliotumiwa maombi na wametoa Seti 100 za Viti na Meza zenye thamani ya Tsh. 6,500,000.00.

 Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya TIB Kanda ya ziwa Bw. Emmanuel Bushiri amekiri kupokea maombi ya msaada wa viti na meza kutoka Halmashauri ya Missenyi na kuamua kuwaunga mkono kwa seti 100 za viti na meza ili kutatua tatizo la vifaa hivyo. “Tunaamini msaada huu utachangia malengo ya Serikali ya kuendelea kuboresha elimu inayotolewa ili iweze kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwa wahitimu wote” Alisema Bwana Bushiri.

Akitoa tahmini ya hali ya upungufu wa viti na meza katika shule za sekondari wilayani hapa, Bi Misinde amesema, awali upungufu wa seti za viti na meza ulikua seti 846 na Halmashauri ilitoa kiasi cha Tsh milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza seti 400 za viti na meza.

Akitoa salamu za shukrani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mh. Projestus Tegamaisho ameishukuru Benk ya TIB kwa mchango huo huku akiwataka wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano huo. “Tunawashukuruni wafadhili wetu kutoka Benki ya Maendeleo ya TIB kwa msaada wa viti na meza, fikira yenu ya kuleta madawati ni fikra sahihi kwani uhitaji ni mkubwa kutokana na ongezeko la wanafunzi…Mh. Mkuu wa mkoa tunaomba uendelee kutupigia debe ili tuendelee kupata zaidi”  alisema Tegamaisho.

Nae mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi msaada wa seti 100 za viti na meza, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameishukuru  Benki ya TIB nakutoa wito kwa walimu kutunza vizuri samani hizo ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

Tarifa Kwa Umma

  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020 January 16, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MISSENYI December 19, 2020
  • MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019 July 09, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • WILAYA YA MISSENYI YAPOKEA SETI ZA VITI NA MEZA 100 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO TIB

    February 09, 2021
  • HALMASHAURI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA SHULE ZA SEKONDARI

    January 25, 2021
  • HALMASHAURI YATOA MKOPO WA TSH. 92,150,000.00 KWA VIKUNDI 15 VYA VIJANA NA WANAWAKE

    October 23, 2020
  • TIMU YA MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YAKAGUA MIRADI 17 YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NDANI YA HALMASHAURI

    October 15, 2020
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa