• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Secondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Mipango Takwimu na Uuatiliaji
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

WIKI YA KAGERA -UJUMBE KUTOKA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Posted on: August 15th, 2019

Wiki ya Uwekezaji Kagera imeanza rasmi mkoani Kagera Agosti 12, 2019 kwa Mabalozi kutoka nchi za ukanda wa Afrika mashariki na kati kueleza fursa zinazopatikana katika nchi walizotoka na namna gani wafanyabiashara wa Kagera na Kanda ya Ziwa wanaweza kuchangamkia fursa hizo.

Mabalozi hao waliwasilisha fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera waliohudhuria kongamano kwa lengo la kuwaonyesha fursa zinazopatikana katika nchi walizopo. Mabalozi wa Tanzania kutoka katika nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamehuzuria kongamano.

Akiwasilisha fursa zinazopatikana Rwanda balozi wa Tanzania Nchini humo Inspekta Jenerali Mstaafu Ernest Mangu ameushauri Mkoa wa Kagera kujenga masoko ya mipakani ili kusogeza bidhaa mbalimbali zinazopatikana nchini kuyafikia masoko ya nchi jirani haraka tofauti na ilivyo sasa kwani wafanyabiashara kutoka nchi za nje wamekuwa wakiingia ndani na kujitafutia bidhaa wenyewe.

Katika hatua nyingine balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dk. Pindi Chana alisema kuwa wafanyabiashara wa Kagera na Tanzania bado wanahitaji Elimu kubwa juu ya biashara za kimataifa huku akitilia mkazo matumizi ya teknolojia za mitandao katika biashara zao badala ya kubeba bidhaa na kwenda kutafuta soko.

Mhe. Dk. Aziz P. Mlima balozi wa Tanzania nchini Uganda amewataka wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera kulima zao la parachichi ambalo sasa lina soko kubwa nchi za nje kuliko kujikita kupanda miti ya mbao pekee.

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dr. Edmund Kitokezi amewataka wafanya biashara nchini kutoiangalia Burundi kwa udogo wake kwani fursa za kibiashara zilizopo Burundi ni nyingi.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Lt. Jen. (mst) Paul I. Mella amewashauri wafanya biashara wa Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla kutumia ukubwa wa eneo na wingi wa watu nchini Kongo kama fursa ya pekee nchini humo. “nchi ya Kongo ina soko kubwa la biashara na si mkoa wa Kagera tu bali Kanda ya ziwa kutokana na ukubwa nchi  na wingi wa watu” alisema Lt. Mella.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kongamano la wafanyabiashara ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amewataka wafanayabiashara wa Kagera kuchangamkia fursa mbali mbali za biashara. “Hapa tunaongelea fursa ya kitaifa na si mkoa wa Kagera tu kwani kati ya nchi nane zinazopakana na Tanzania nchi nne zote zinapakana na Mkoa wa Kagera kwa hiyo mkoa huu ni kitovu cha uchumi wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati nataka kuona hamasa ya wafanya biashara wetu hapa wakitumia fursa hiyo.” Alisistiza MKuu wa Mkoa Gaguti

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju hakusita kutoa aliyo nayo kwa wafanya biashara wa mkoa wa kagera huku akiwataka wachangamkie fursa ya uongozi awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuri ambao ni rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. “Mkoa wa Kagera sasa ni wakati wake wa kuinuka kiuchumi katika Awamu hii ya Tano na uongozi wa Mkoa usiruhusu malumbano ya kiasiasa kukwamisha maendeleo pia usiruhusu wafanyabiashara wabinafsi kuhodhi biashara wao peke yao” alisisitiza Mh Mpanju.

Akitoa shukrani kwa mabalozi hao kuja katika kongamano Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Wilfred Lwakatare amesema mabalozi hao ni sawa tu wametoa cheki ya fedha iliyo wazi kwa wafanya biashara na wananchi kwa ujumla na kilichobaki ni wao tu (wafanya biashara) kuandika kiasi chochote cha fedha wanachohitaji.

Tarifa Kwa Umma

  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020 January 16, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MISSENYI December 19, 2020
  • MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019 July 09, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YATOA MKOPO WA TSH. 92,150,000.00 KWA VIKUNDI 15 VYA VIJANA NA WANAWAKE

    October 23, 2020
  • TIMU YA MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YAKAGUA MIRADI 17 YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NDANI YA HALMASHAURI

    October 15, 2020
  • HALMASHAURI YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVu

    September 05, 2020
  • KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AZINDUA RASMI UJENZI WA MRADI WA MAJI WA KYAKA-BUNAZI

    June 01, 2020
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    BUNAZI MISSENYI KAGERA TANZANIA

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 38 KYAKA MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: 0732983531

    Namba ya simu :

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa