• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Secondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Mipango Takwimu na Uuatiliaji
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

HALMASHAURI YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVu

Posted on: September 5th, 2020

Na Mwandishi wetu.

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi imeendelea kutekeleza lengo la kuboresha hali ya maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa vikundi 23 kwa vijana, wazee na walemavu kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/2020. Mikopo hiyo ni kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha asilimia kumi ya mapato ya ndani yanatengwa kwa ajili ya kuwawezesha wajisiliamali wanawake, vijana na walemavu kutekeleza shughurizao za ujasiliamali wenye tija.

Katika hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake,vijana na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya WIlaya ya Missenyi leo Septemba 5/2020 jumla ya Kiasi cha Tshs 82,750,000.00 zimekopeshwa kwa jumla ya vikundi 23 ikiwa ni vikundi 18 vya wanawake (Tsh 58,000,000.00), vikundi vinne vya vijana (Tsh 21,750,000.00) na kikundi kimoja cha watu wenye ulemavu (Tsh. 3,000,000.00). Mikopo hii inatarajiwa kurejeshwa na vikundi husika ndani ya mwaka mmoja  na haina riba.

Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ililenga kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu yenye thamani ya Tshs. 194,220,000.00. Hadi juni 2020, Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya Tshs. 194,220,000.00 sawa na asilimia 100 ya lengo la mwaka.

Akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo kwa vikundi, Afisa maendeleo ya jamii Bi. Beatrice Sanga amesema manufaa yanayotarajiwa baada ya kutoa mikopo hii ni pamoja na kuwezesha vikundi kupanua mitaji, kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitakazo kidhi mahitaji ya soko na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa walengwa. Manufaa mengine ni kuchochea utengenezaji na upatikanaji wa ajira kwa vijana, kuwaepusha wanufaika na vitendo hatarishi vinavyochochea mmomonyoko wa maadili na uvunjifu wa amani, ukuaji wa uchumi wa kaya na jamii na kupunguza umasikini.  Pia Halmashauri itaongeza mapato kupitia vyanzo vyake vinavyoelekeana na shughuri za wajasiliamali.

Bi Sanga ametaja changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza  katika utoaji wa mikopo ni pamoja na baadhi ya wakopaji kukosa uaminifu kwa kukiuka mikataba , vikundi kubadili matumizi ya fedha walizokopeshwa kinyume na maandiko waliyowasilisha wakati wa kuomba mikopo na mwitikio mdogo wa vijana kuanzisha miradi ya pamoja yenye tija na kuomba mikopo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Missenyi  Col. Denis Filangali Mwila ambaye pia ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo , amevitaka vikundi vilivyopokea mikopo hiyo hasa vijana kuitumia mikopo hiyo kwa lengo lililokusudiwa na kuonyesha mfano wa kuigwa kwa vijana wengine na si kuitumia mikopo hiyo kwa namna isiyo faa.

Ili kufanya zoezi la utoaji mikopo kwa vikundi liwe endelevu,  Halmashauri imeendelea kusimamia urejeshaji wa mikopo kwa vikundi vilivyonufaika kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na utoaji wa elimu kwenye vikundi husika ili watumie fedha kwa malengo yaliyokusudiwa. Hii itaondoa tatizo la vikundi kufanya matumizi ya fedha za mikopo yasiyoendana na malengo ya mikopo. Sambamba na hilo uhamasishaji umeendelea kufanyika ili vijana wajiunge kwenye vikundi na kuanzisha miradi yenye tija kusudi wapate sifa ya kuomba mikopo inayotolewa na Halmashauri.

Tarifa Kwa Umma

  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020 January 16, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI April 01, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MISSENYI December 19, 2020
  • Tazama zote

Habari mpya

  • TSH.MILIONI 139.2 ZATOLEWA KWA MAKUNDI YA VIJANA WANAWAKE NA WALEMAVU

    March 09, 2021
  • WILAYA YA MISSENYI YAPOKEA SETI ZA VITI NA MEZA 100 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO TIB

    February 09, 2021
  • HALMASHAURI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA SHULE ZA SEKONDARI

    January 25, 2021
  • HALMASHAURI YATOA MKOPO WA TSH. 92,150,000.00 KWA VIKUNDI 15 VYA VIJANA NA WANAWAKE

    October 23, 2020
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa