• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
MISSENYI DISTRICT COUNCIL
MISSENYI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Missenyi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Secondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Mipango Takwimu na Uuatiliaji
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Kiuchumi
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Kudhibiti ukimwi
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayo Tekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha mbalimbali

TAARIFA YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO 2015 – 2020

28 June 2020

HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI

 
 


 

TAARIFA YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KIPINDI CHA  MIAKA MITANO (2015 – 2020).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha Siku ya leo. Aidha mtakumbuka kuwa kuna wezetu tulianza nao katika Baraza hili mwaka 2015 lakini kufikia sasa hatupo nao wametutoka. Niwaombe tusimame kwa dakika moja kuwaombea. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, Napenda kuchukua fursa hii tena kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kutuongoza na kuendelea kuijali Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zake katika Sekta za Maji na Barabara; Tunasema asante sana – Tunamwombea aendelee kuongoza. Vile vile nichukue fursa hii  kutoa shukrani za dhati kwako Mheshimiwa Mwenyekiti na wajumbe wote wa Baraza, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Katibu Tawala Mkoa, Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji,  Viongozi wa chama tawala (CCM) pamoja na wadau wote wa maendeleo kwa Ushirikiano mkubwa mliotupatia  kwa kipindi chote hadi leo tanapohitimisha Baraza hili.  

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kikao cha leo ni kikao maalum kwa ajili ya kuwawezesha Waheshimiwa Madiwani kujadili na kupitisha mambo Muhimu ambayo yanahitaji ridhaa yetu na Pia, kutafakari tulipotoka na tulipo ili tuweze kuwa Nguvu, Ari na Mwelekeo mpya katika kuwatumikia Wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo yaani 2020/2021 – 2024/2025 kwa madhumuni ya kuendeleza lengo letu kama wana Missenyi kushiriki moja kwa moja kufanikisha Tanzania ya Viwanda na hatimaye kuifikisha kwenye Uchumi wa kati ifikapo 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka mitano, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imetekeleza ilani katika maeneo yote muhimu kwa zaidi ya asilimia 95 katika Nyanja za Ukuaji wa Uchumi, Uzalishaji mali, Huduma za Kiuchumi, Huduma za Jamii, Uwezashaji wananchi kiuchumi na Ukuzaji wa utawala wa Kidemokrasia na Utawala Bora.

 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Mwaka 2015/2016 tulipokuwa tunaingia Madarakani tulikuwa na Bajeti ya Tsh. 21,565,000,353.95 na mwaka 2019/2020 tumeweza kuongeza bajeti ya Mapato na Matumizi hadi kufikia Tsh. 25,257,247,645.00. Mapato na Matumizi hayo yamengezeka kwa Tsh, 3,692,247,291.05 sawa na asilimia 17. Ongezeko hilo limetokana mikakati madhubuti ya kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani baada ya Serikali Kuu kupunguza fedha za Matumizi Mengine pamoja na Mishahara ya Watumishi wasiokuwa na sifa za kuendelea na ajira za Serikali kwa ajili ya changamoto za kiutumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Mapato ya ndani ya Halmashauri kama Sehemu ya Bajeti kuu yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Halmashauri ilikisia kukusanya na kutumia kiasi cha Tsh. 1,233,744,000.00 na kukusanya na kutumia Tsh. 1,135,686,580.00 sawa na asilimia 92 ya maksio ya mwaka.

Hata hivyo kutokana na Mahitaji ya huduma za Kiuchumi na Kijamii kwa Wananchi wa Missenyi kuendelea kuongezeka siku hadi siku na dhamira yetu ya kutaka kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 50 ifikapo 2025 ndipo, Mwaka 2016/2017 Baraza letu hili la Madiwani lilitengeneza Kanzi data ambayo ilipelekea kuongeza mapato ya Halmashauri.

Mwaka fedha 2019/2020, Halmashauri ilikisia kiasi cha Tsh. 2,467,613,000.00 na hadi tarehe 28.05.2020 imekusanya Tsh. 2,480,130,014.72 sawa na asilimia 100 na hadi tarehe 8.06.2020 tumeweza kukusanya Tsh.2,532,880,626.65 sawa na asilimia 102.6 ya maksio ya Mwaka. Lengo letu kubwa ni kuendelea kupunguza utegemezi toka Serikali Kuu ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 tumepanga kukusanya Tsh. 3,041,629,000.  

Aidha kwa mikakati tuliyojiwekea tunatarijia ifikapo Mwaka wa fedha 2024/25 tuweze kukusanya zaidi ya bilioni tano. Kwa kuwa na kiasi hicho, Halmashauri itaweza kupunguza utegemezi toka Serikali kuu kwa zaidi ya asilimia 40 katika Shughuli za uendeshaji wa Ofisi na Miradi ya Maendeleo. 

Kwa upande wa matumizi, Halmashauri imeendelea kufanya vizuri ambapo kwa muda wa miaka minne imepata hati safi yaani kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2018/2019, Aidha tulipoingia madarakani Halmashauri ilikuwa na Hati yenye Mashaka na tumemaliza Halmashauri ikiwa na Hati safi hongereni sana kwa ushirikiano huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Kwa kipindi cha miaka mitano yaani 2015 hadi 2020, Halmashauri imeweza kutekeleza miradi 430 ya Maendeleo yenye thamani ya Tsh. 14,366,582,275.74, ikiwa miradi ya Serikali Kuu ni Tsh. 7,078,818,000/= Miradi ya Mapato ya ndani ni Tsh. 2,812,425,954/=, Miradi ya Wadau wa Maendeleo ni Tsh. 2,280,719,715, Miradi ya Mfuko wa Jimbo ni Tsh. 255,340,000.00 na Tsh. 1,939,278,606.74 ni Michango ya Jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kwa upande wa Sekta za uzalishaji mali, Halmashauri imetoa kipaumbele ambapo kwa upande wa Kilimo imeweza kuhamasisha wananchi kuongeza mazao ya Chakula na Biashara kama vile, Mahindi, Maharage, Mpunga, Vanila, Alizeti  na Kahawa; Mathalani uzalishaji wa mazao ya chakula  umeongezeka kutoka tani 152,886  (Mwaka 2015) hadi tani 202,544.3 Mwaka 2019. Jambo hili limewesha Wananchi wa Wilaya ya Missenyi kuwa na chakula cha kutosha ambapo chakula cha ziada kimeweza kuuzwa kwa ajili ya kujipatia fedha za kuendesha maisha ya familia zao.

Kuongezeka kwa maeneo ya kulima nalo ni moja ya mafaniko yetu, Mfano wa zao moja la chakula la Mpunga mwaka 2015 tulikuwa tunalima Hekta 12 lakini mwaka 2020 tunalima hekta 39.04. Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya biashara ya Miwa na Kahawa kwa zaidi ya tani 10,000 kwa kipindi cha miaka mitano, pia zao la Vanila limeongeza kutoka miche 40,401 hadi 101,111. 

Kwa upande wa Mifugo, Halmashauri imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafugaji ambapo Halmashauri imeendelea kupokea ruzuku ya dawa za kuogeshea mifugo, Kusimamia utoaji wa chanjo na uhimilishaji wa Ng’ombe kutoka Ng’ombe 231 (2015/2016) hadi 694 (2019/2020). Kutokana na uboreshaji huo uzalishaji wa mazao ya mifugo umeongezeka kutoka tani za Nyama 474 (2015/2016) hadi 517 (2019/2020) na Maziwa Tani 9,972,984 (Mwaka 2015/2016) na 12,252,626 Mwaka 2019/2020. 

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Halmashauri ina maeneo yenye wingi wa rasilimali za uvuvi ambazo ni Sehemu ya Ziwa Victoria, Mto Kagera, Mto Ngono, maeneo Oevu na Mabwawa ya ufugaji wa Samaki, Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mafanikio mengi yamepatikana ikiwa ni pamoja na vyombo vya uvuvi kuongezeka kutoka 36 mwaka 2015/2016 na hadi kufikia 62 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 72, Ajira za Uvuvi zimeongeka kutoka 217 mwaka 2015/2016 hadi kufikia ajira 274 mwaka 2019/2020, Samaki tani 49 zenye thamani ya Tsh. 245,000,000.00 walivuliwa kwa mwaka 2015/2016 na samaki Tani 120.2 zenye thamani Tshs 721,452,000.00 walivuliwa kwa mwaka 2019/2020. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 143.

Vile vile Sekta ya Uvuvi ilikuwa inachangia mapato ya Halmashauri kiasi cha Tshs 5,518,600.00 kwa mwaka 2015/2016 ukilinganisha na kiasi cha Tshs 19,533,400.00 kwa mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 254. Usimamizi wa rasilimali za uvuvi katika ziwa victoria umeimarishwa ambapo, Kwa kipindi cha miaka mitano, Doria za kawaida 22 zimefanyika kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu na kudhibiti upotevu wa maduhuli ya mapato ya Serikali katika maeneo mbalimbali ambapo zana haramu, nyavu 963 zenye thamani ya Tshs. 95,616,000.00 zimeteketezwa.

 

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mabwawa ya ufugaji wa Samaki yameongezeka kutoka 25 mwaka 2015/2016 hadi 51 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 104.

Kwa upande wa Maliasisili, Halmashuari imeendelea kutekeleza kwa vitendo utunzaji wa Misitu na Mazao yake ambapo imeweza kupanda miti 11,084,302 kwa kipindi cha miaka mitano, kati ya hiyo watu binafsi wamepanda miti 8,247,155, Vikundi miti 1,342,400 na Taasisi ni miti 1,494,747. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kwa upande wa Usafi na Mazingiza, Halmashauri imweza kutoa elimu ya usafi na Mazingira kwa Vijiji vyote 77 ikiwa ni pamoja na kujenga vizimba 3 vya kukusanyia takataka ngumu katika miji ya Kyaka na Bunazi, kuwa na Sheria ndogo ya usimamizi wa taka; kuanzisha mfumo wa ada ya taka ambapo chanzo hicho kinaingiza zaidi ya Tsh. 1,500,000/= kwa mwezi na fedha hiyo imekuwa msaada mkubwa wa kufanikisha shughuli za Usafi na Mazingira, Kuongeza Vyoo bora kutoka asilimia 37 ya mwaka 2015 hadi asilimia 82 ya Mwaka 2020. Hali ya utuzaji na uhifadhi wa Mazingira kwa Wilaya umeongezeka kutoka asilimia 54 Mwaka 2015 hadi asilimia 85 mwaka 2020 ambapo kila Kijiji kina sheria Ndogo za kuhifadhi na kutunza Mazingira ambazo zilipitishwa na Baraza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kutokana na juhudi hizo kubwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imefanikiwa kuwa mshindi wa tatu kitaifa kwa Mwaka 2019 na Kupewa cheti na fedha kiasi cha Tsh. 5,000,000/= ambazo zimetumika kununulia pikipiki kwa ajili ya kuwaezesha maafisa Usafi na Mazingira kuwa na usafiri wa uhakika, Pia Halmashauri imeweza kutoa Kijiji cha Kitobo kama Mshindi wa tatu kitaifa katika kazi ya Vijiji na kuzawadiwa Tsh. 1,000,000/=. 

Kwa upande wa uwekezaji, Halmashauri imeweza kutenga zaidi ya Hekta 5,250.5 kwa ajili ya Kilimo, Biashara na Viwanda. Kwa Upande wa Viwanda Vikubwa, Vya Kati na Vidogo idadi imeongezeka kutoka 61 vya Mwaka 2015/2016 hadi kufikia 98 mwaka 2019/2020 sawa na asilimia 62 hivyo kuongeza ajira ya Watumishi rasmi kutoka 1,620 mwaka 2015/2016 hadi kufikia Watumishi 2,040 mwaka 2019/2020. Kwa mantiki hiyo ongezeko hilo limechangia kukuwa kwa sekta ya Biashara kutoka asilimia 40 ya Mwaka 2015 hadi asilimia 70 Mwaka 2020. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kwa upande wa Sekta  Wezeshi za Kiuchumi, Halmashauri imeweza kutoa hati miliki kwa Vijiji 46, kuandaa mpango wa matumizi bora kwa Vijiji 12, Kutoa hati za kimila 715 na kuongeza  Viwanja vilivyopimwa kutoka 1,498 vya mwaka 2015/2016 hadi kufikia 2,552 mwaka 2019/2020. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 41.

Sekta ya Barabara imendelea kuimarika ambapo barabara zenye urefu wa kilometa 656.93 zimekuwa katika hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kilometa 621.93 zimekamilika kwa kujengwa kwa kiwango cha Changarawe na Udogo na kupitia wakala wa barabara Vijijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imepokea kiasi cha  Tsh. 2,962,023,812 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aidha, kwa mwaka 2019/2020 barabara zenye urefu wa kilometa 77.98 km zimeendelea kujengwa kati ya hizo 1.6 km ni kiwango cha lami kwa gharama ya Tshs. 741,972,480 ikiwa ni ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jimbo la Nkenge na 76.36 km ni kiwango cha changarawe na udongo kwa gharama ya Tsh. 407,521,200.00

Kwa upande wa Sekta ya Umeme, Tunapenda kuishukuru kwa dhati Serikali ya Awamu ya Tano ambapo kiwango cha uunganishaji wa Umeme kimeongezeka kutoka Vijiji 26 (Mwaka 2015) sawa na asilimia 33.7 hadi kufika Vijiji 72 (Mwaka 2020) sawa na asilimia 93.5. Katika uunganishwaji huo wa umeme wa REA Nyumb a za Makazi ni zaidi ya 3,326, Nyumba za ibada ni 26, Shule ni 43 na zahanati ni 11 zimenufaika.

Hakika Kwa sasa wananchi wa Missenyi usiku kwao ni kama mchana!!

 

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Halmashauri hii pia ilijikita katika kuhakisha kuwa huduma za Jamii zinaboreshwa,  ambapo Sekta ya Afya tumeweza kukarabati  kituo cha Afya cha Bunazi kwa gharama ya Tsh. 437,950,350.00 na sasa huduma za upasuaji wa kinamama wajawazito zinatolewa, Kujenga kituo cha Afya kipya cha Kyabaile, Kujenga Zahanati moja ya Ngando, hivyo kufanya Halmashauri kuwa na Vituo 2 vya Afya vya Serikali, Kutenga na kupima eneo kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, Kuongeza huduma ya kliniki  zinazohamishika (Huduma ya mkoba) kutoka 35 Mwaka 2015 hadi 95 Mwaka 2020 sawa na asilimia 171, Kuongeza Watumishi wa Afya kutoka 271 mwaka 2015 hadi 382 mwaka 2020 sawa na asilimia  41 na kuongezeka kwa bajeti ya dawa  na vifaa tiba kutoka Tsh. 281,763,765/= Mwaka 2015/2016 hadi 593,837,525.60 sawa na asilimi 111. 

 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kwa upande wa Elimu Msingi, Halmashauri imeweza kuandikisha watoto wa darasa la awali kutoka 6,116 (2015) hadi 7,686 (2019) sawa na asilimi 25.6, Darasa la kwanza kutoka 6,107 mwaka 2015 hadi 6,993 mwaka 2019 sawa na asilimia 14, Nyumba za Walimu kutoka 205 (2015 hadi 217 (mwaka 2017), Matundu ya vyoo kutoka  901 (Mwaka 2015) hadi kufikia 1,087 Mwaka 2020 sawa na asilimia 20.6, Madawati yameongezeka kutoka 13,116 Mwaka 2015 hadi kufikia 19,987 mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 52.3 na kufanya ufaulu kuongezeka kutoka asilimia 75.5 mwaka 2015 hadi 84.8 mwaka 2019 na kuwesesha ununuzi wa Photocopy mashine 1 kubwa ambayo itawezesha sasa Watoto wetu kuondokana na mitihani ya kuandikiwa ubaoni na kuwa na mitihani ya mwezi na mihula iliyochapishwa kwa grarama nafuu, Tumefanya hivi ili kuwa uendelevu wa Ufaulu kwa watoto wetu wa Shule za Msingi. Sekta hii imepokea Tsh. 1,922,702,700.72 kwa Ruzuku ya Wanafunzi na Posho ya Madaraka toka Disemba, 2015.

Kwa upande wa Elimu ya Ufundi, Udahili wa Wanafunzi katika Chuo cha Ufundi Gera umeongezeka kutoka Wanachuo 43 Mwaka 2015 hadi Wanachuo 173 mwaka 2020 sawa na asilimia 302 ikiwa ni sambamba na ukarabati wa Madarasa, Mabweni na jengo la Utawala. Aidha chuo kinaendelea na utengenezaji wa Miundombinu ya ufugaji wa Nyuki kwa ajili ya Mafunzo kwa Jamii yetu hususani Vijana. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kwa upande wa Elimu Sekondari, Halmshauri imeweza kuongeza idadi ya Walimu kutoka 242 mwaka 2015 hadi kufikia 379 mwaka 2020 na kuwa na idadi kubwa ya walimu wa Sanaa, hivyo Walimu 96 wa Sanaa walihamishiwa shule za Msingi, kuongeza Walimu wa Sayansi kutoka 54 Mwaka 2015 hadi 90 mwaka 2020 sawa na asilimi 67, Kuongeza Vyumba vya Maabara kutoka vyumba 7 hadi 46 Mwaka 2020 sawa na asilimia 557 na na Maabara 20 zipo katika hatua mbalimbali za Ujenzi ambapo zinategemewa kukamilika kabla ama ifikapo Juni, 2021;

Matundu ya Vyoo yameongezeka kutoka 311 mwaka 2015 hadi 335 mwaka 2020 sawa na asilimia 8, Seti za Viti na Meza 8,646 mwaka 2015 hadi 9,283 mwaka 2020, Kupokea Vifaa vya Maabara vya Masomo ya Kemia, Fizikia na Biolojia kwa Maabara 37 za Sekondari 13. Aidha Halmashuri imepokea Kiasi cha Tsh 632,626,305/= kama fidia ya ada, Tsh. 402,342,993/= Ruzuku ya uendeshaji na Tsh. 313,500,000/= ni Posho ya Madaraka kwa Wakuu wa Shule zote. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Sekta ya Maji, Huduma ya Maji imeongezeka kutoka asilimia 58 ya Mwaka 2015 hadi asilimia 71 ya Mwaka 2020 ambapo miradi ya Rukurungo, Igurugati, Kenyana, Bulembo, Kashaba, Nyankere, Kibeo, Bugango, Kakunyu, Kakindo, Razinga na Bulfani ndio iliongeza ongezeko hili, Miundombinu 9 ya maji inayotoa maji safi kwa wananchi imekamilika pamoja na visima virefu 23, Visima vifupi 243, vyanzo vya maji 10 na Matenki 48 ya kuvuna maji ya mvua.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi imetekeleza kwa Vitendo sera ya kuwezesha Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ambapo wajasiliamali 4,080 wametambuliwa na Jumla Tsh. 501,995,546 imetolewa kama mkopo kwa Vikundi 262 ikiwa vya Wanawake ni 158, Vijana 91, na Walemavu ni 13, Mikopo hii isiyokuwa na riba imewezesha wananchi wa Missenyi 3,302 kupata ajira kupitia asilimia 10 ya mapato halisi ya Halmashauri kwa kipindi cha miaka 5 yaani 2015 - 2020.

Aidha, Mtakumbuka kuwa tulipokuwa tunaingia Madarakani yaani mwaka 2015/2016 Halmashauri ilikuwa inapeleka kiasi Tsh. 12,000,000/= kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu lakini sasa wakati tunatoka Madarakani zimeweza kupekeka kwa asilimia 100 kiasi cha asilimia 10 ya mapato halisi ya ndani, mathalani kwa Mwaka 2019/2020 pekee tumepeleka hadi sasa kiasi cha Tsh. 193,104,605/= na bado mwaka wa fedha haujaisha, Hivyo ni matajio yetu sote kuwa mpaka Juni, 30, 2020, Halmashauri itapeleka zaidi ya Tsh. 200,000,000/=,

Pia Halmashuri imewezeshwa na ofisi ya Waziri Mkuu kujenga jengo la Kitalu Nyumba kwa ajili ya Vijana kujifunza na kujiajiri ambapo Vijana 100 walipata mafunzo ya nadharia na Vitendo. Aidha, Halmashauri imwezea kuhamasisha uanzishwaji wa VICOBA kutoka 19 mwaka 2015 hadi 155 mwaka 2020 vyenye Wanachama 4,240 hai

Kwa upande wa kuwezesha Kaya masikini, Halmashauri kupitia mfuko wa TASAF imepokea na kulipa Tsh. 5,141,704,500/= kwa kaya 6,292. Kaya hizo zimeweza kuandikisha kliniki watoto wenye umri wa miaka chini ya mitano kutoka 3,370 mwaka 2015 hadi 4,755 mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia 41, kuandikisha watoto shule kutoka 3,127 mwaka 2015 hadi 5,623 mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 80, kujiunga na bima ya Afya kwa hiari kutoka kaya 1,234 mwaka 2015 hadi 3,026 mwaka  2019.

Pia kuanzisha Miradi ya ufugaji mdogo mdogo wa kuku 11,624, Mbuzi 618, Nguruwe 1,022 hivyo kaya 3,267 kati ya 5,703 sawa na asilimia 57 wanafuga, Kuanzisha kilimo ambapo kaya 5,402 kati ya 5,703 sawa na asilimia 95 wanatumia sehemu ya ruzuku kwa ajili ya kuongeza kipato na kuwa na uhakika wa chakula kwa zaidi ya asilimia 76, kaya 106 kati ya 5,703 sawa na asilimia 1.9 zinajishughulisha na biashara ndogondogo.

Vile vile Nyumba 451 zimejengwa na kukarabatiwa na Wanufaika na kaya 402 zimenunua mabati 2,530 kwa ajili ya ujenzi. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Wadau wa maendeleo katika Halmashauri yetu wamekuwa kiungo muhimu sana katika utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo, Nichuke fursa hii kuwashukuru kwa kazi nzuri walioifanya kwa kipindi chote cha miaka mitano. Kwa kutambua mchango wao tumeandaa vyeti vya shukrani ambavyo naomba uvitoe kwa wadau 34 kama ifuatavyo:- World Vision – Missenyi ADP; Missenyi AIDS and Poverty Eradication Crusade (MAPEC); Management and Development fo Health (MDH); International Center for Disease/AIDS Intervention Programme (ICAP); Tanzania Development and AIDS Prevention Association (TADEPA); PARTAGE Tanzania; Shirika la Matumaini na Maendeleo Kanyigo (SMMK); Kikukwe Community Development Initiative (KCDI); Concern for Community Resources Development (CCRD); ARK Missenyi Youth Development Network; ELCT,  North Western Diocise; Roman Catholic Church, Bukoba Diocise; BAKWATA Missenyi; Compassion International Tanzania (CITZ); John Snow Inc (JSI); IMA World Health; Marie Stopes; JPIEGO; Population Service International (PSI); IntraHealth; Umoja wa Wasaidizi wa Kisheria Missenyi (UWASHEMI); Jambo for Development (JFD); KADERES; Matumaini Mapya; Read Cross; Ruzinga for Development; St. John Catholic Church Wahpeton, North Dankest, USA; Redio Karagwe, Kagera Community  Radio (KSR); Mkuu wa Wilaya Missenyi; Vijana – Tuinuane Kilimo – Kijiji cha Byamutemba , Kata  ya Nsunga, Walemavu -  Tujitegemee  wenye ulemavu  - Kijiji cha Kashekya, Kata ya Gera; Wanawake – KAOFACO  - Kijiji cha Bunazi  kata  ya Kassambya na Kagera Sugar ltd.

 

Mheshimiwa Mwenyekiti, 

Kwa namna ya pekee nichukue tena fursa hii adhimu kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutupatia Afya njema hadi siku ya leo. Vile vile niwashukuru wajumbe kwa ushirikiano mliotupatia toka mlipoingia Madarakani. Aidha, niendelee kutoa shukrani za dhati kwa Wadau wa Maendeleo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Ofisi ya CCM Wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wizara zote kwa ushirikiano na Kipekee Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Nasema ahsanteni sana!!!

Tarifa Kwa Umma

  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020 January 16, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MISSENYI December 19, 2020
  • MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019 July 09, 2019
  • Tazama zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YATOA MKOPO WA TSH. 92,150,000.00 KWA VIKUNDI 15 VYA VIJANA NA WANAWAKE

    October 23, 2020
  • TIMU YA MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YAKAGUA MIRADI 17 YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NDANI YA HALMASHAURI

    October 15, 2020
  • HALMASHAURI YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVu

    September 05, 2020
  • KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AZINDUA RASMI UJENZI WA MRADI WA MAJI WA KYAKA-BUNAZI

    June 01, 2020
  • Tazama zote

Video

Video nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Sheria ndogo za Halmashauri

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Mkoa Kagera
  • Tovuti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Serikali Kuu
  • Tovuti ya TAMISEMI

Watembeleaji walipo

world map hits counter

Waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    BUNAZI MISSENYI KAGERA TANZANIA

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 38 KYAKA MISSENYI

    Namba ya Simu ya mezani: 0732983531

    Namba ya simu :

    Barua pepe: ded@missenyidc.go.tz

Anuani zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki @2017 Wilaya ya Missenyi. Haki zote zimehifadhiwa